Katika hali ya kawaida watu wengi wamezoea kusikia na kuambiwa kuwa
Chocolate si kitu kizuri na kuna sababu nyingi za kukufanya uamini kuwa
chocolate si nzuri.
Watu husema inaharibu meno, wengine hudai kuwa
inasababisha kisukari na wengine huenda mbali zaidi wakidhani kuwa inaharibu ngozi
kutokana na wingi wa mafuta iliyo nayo.
Watoto wadogo ambao wamezoeleka kuwa wapenzi wakubwa wa
chocolate ndio huvunjwa moyo na wazazi/walezi wao katika hili.