Thursday 12 March 2015

Makosa 10 ya kuepuka ili upate mafanikio ya kipesa


Pesa ni chombo kinachotumika kupima thamani ya vitu kama huduma na bidhaa. Pesa hutumika kubadilisha bidhaa na huduma mbalimbali. Kupata na kuhifadhi pesa imekuwa ni changamoto kubwa sana. Hivyo basi ili uweze kufanikiwa yakupasa kujifunza kuhusu pesa. Watu wengi waliofanikiwa wamejifunza na kuelewa pesa.
  1.  Matumizi yasizidi mapato
Ili uweze kufanikiwa kimaisha hasa katika suala la pesa, basi yakupasa kutumia pesa chini ya kiwango unachoingiza. Hii itakusaidia kuweka akiba kwa matumizi ya baadae na
hata kuwekeza. Jifunze kuwa na nidhamu ya pesa ikiwa ni pamoja na kuhifadhi angalau 10% ya pato lako. Watu wengi waliofanikiwa wanalijua hili vyema.
  2.  Kujua thamani ya vitu.
Yakupasa ujue thamani ya vitu unavyotakiwa kuwa navyo. Japokuwa uwekezaji ni muhimu, lakini lengo la kuwekeza ni kuweza kutimiza mahitaji yako ya kila siku mfano chakula, mavazi na hata malazi. Unatakiwa kununua vitu vyenye ubora wakati wote ili viweze kudumu. Ukipenda kununua vitu vyenye ubora mdogo kwa thamani ndogo utajikuta ukinunua mara nyingi na hivyo kupoteza pesa zaidi ya aliyenunua kimoja cha thamani. Kumbuka gharama ya kitu huendana na thamani yake.
  3.  Kutobweteka na mapato yasiyoongeeka
Ili uweze kufanikiwa inakupasa kuhakikisha kwamba mapato yanakuwa siku hadi siku na kutoridhishwa kipato kisichokuwa. Inakupasa kutafuta vyanzo vipya vya pesa ili uweze kuongeza kipato chako vinginevyo utafilisika si muda mrefu. Pia yakupasa kujifunza jinsi ya kukuza biashara zako.
  4.  Kutopuuzia hati za pesa (financial statements)
Hakikisha unakagua hati zako za kibenki kila mara ili uweze kujua mapato na matumizi yako,  Pia miradi, uwekezaji na miamala mingine. Hii itakusaidia kugundua makosa na kuyarekebisha haraka iwezekanavyo. Pia zitakuonyesha kama unakua, umedumaa au unaporomoka. Tenga muda wa kukagua angalau mara moja kwa mwezi.
     5.  Kutokuwekeza kipumbavu
Ili ufanikiwe kipesa yakupasa kuchunguza unachowekeza kabla hujawekeza. Hii itakusaidia sana kutopoteza pesa. Warren Buffet aliwahi kusema ;`Sheria namba moja ni kutopoteza pesa’. Hii haimaanishi kwamba usiwekeze la hasha, bali wekeza unapoona kuna mafanikio. Take calculated risks.
     6.  Usijifanye mjuaji katika masuala ya pesa
Watu wengi waliofanikiwa hawajifanyi wanajua kila kitu hasa linapokuja suala la pesa. Ujue dunia inabadilika kwa kasi mno na hivyo kutakiwa kujifunza mambo mapya kila siku . Watu waliofanikiwa husoma vitabu vihusuvyo pesa na kusikiliza vitabu sauti (audio books) kila mara. Kumbuka elimu kubwa ipo katika vitabu na watu waliofanikiwa.
     7.  Kusikiliza ushauri wa wataalamu wa pesa
Ili uweze kupanda katika kilele cha mafanikio ya pesa yakupasa kutafuta na kuufanyia kazi ushauri wa wataalamu wa masuala ya pesa. Mathalani kupata ushauri kuhusu masula ya kodi, uhasibu na hata masuala ya kisheria.
     8.   Kutokuwa mtumwa wa pesa
Watu hutafuta pesa ili ziwasaidie katika mambo mbalimbali. Kupuuzia vitu vingine vya msingi kisa pesa ni makosa makubwa. Mfano kutokujali afya, chakula, makazi na hata malazi  na elimu yako na jamii yako. Jitathmini kama uko ndani ya malengo yako, taaluma yako, malengo ya kifamilia na malengo mengine ya kimaisha uliyojiwekea.
    9.  Kutokukusahau kurekebisha matumizi ya pesa kunapotokea mabadiliko katika maisha
Katika maisha ya binadamu, mabadiliko ni kitu ambacho hakiepukiki. Mabadiliko yaweza kuwa ndoa, kusomesha nk. Yakupasa kukaa meza moja na wataalamu angalau mara moja kwa mwaka ili uweze kufanya tathmini hali yako ya kifedha.
    10.  Kutokuishi kwa mikopo
Matumizi yako yanapozidi kipato chako itakupasa uanze kuishi kwa kukopa. Hivyo basi jifunza kuwa na nidhamu ya fedha. Watu wengi waliofanikiwa wamekuwa na nidhamu kubwa sana kipesa na wale ambao hawajafanikiwa ni kinyume chake.Mathalani kipato chako ni shilingi 100,000 kwa mwezi lakini matumizi yako ni sh. 250,000 hakuna jinsi utakayokwepa kukopa.
asante kwa kusoma

0 comments:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.