Utangulizi
Maziwa ya soya ni maziwa yanayotokana na mbegu za soya. Ni kinywaji
kizuri kwa afya na pia hutumika kama kiburudisho. Maziwa ya soya hufanana sana
na maziwa ya wanyama hasa ya ng’ombe katika virutubisho na pia mwonekano (rangi).
Maziwa ya soya ni mazuri sana kwa sababu hayana lehemu (cholesterol),mafuta
yasiyofaa/mgando (saturated fats) na yana virutubisho vingi. Maziwa haya hufaa
sana pia kwa watu wenye mzio (allergy) na maziwa ya wanyama kutokana na kukosa
kimeng’enyo kiitwacho lactose (lactose intolerant people).
Jinsi ya kuandaa
1)
Chambua soya zako kuondoa uchafu.
3)
Loweka soya zako kwa muda wa saa 8
au usiku mzima ili kulainisha na pia kuondoa sumu(anti-nutritional factors).
4)
Chemsha soya zako vizuri.
5)
Epua na fikicha kwa vidole kuondoa
maganda.
6)
Ondoa maganda kwa kutumia maji ya
baridi
7)
Kausha soya zako na uzisage ili
kupata unga.
8)
Changanya kikombe kimoja cha unga
wa soya na vikombe 3 vya maji.
9)
Chemsha mchanganyiko wako kwa muda
usiopungua dakika 30.
10)
Epua na chuja mchanganyiko wako
kwa kitambaa safi kuondoa makapi ya soya.
11)
Ongeza sukari na viungo kama
iliki, vanilla n.k.
12)
Pooza maziwa yako na yatakuwa
tayari kunywewa.
Njia nyingine
Fuata hatua zote mpaka hatua ya tatu.
4. Ponda ponda
soya kupata uji uji mzito.
5. Chuja mchanganyo kwa kutumia kitambaa safi.
6. Chemsha mchanganyo wako kasha uuweke kwenye
vyombo safi.
7. Ongeza maji
kuweza kupata maziwa yako ya soya
8. Ongeza
sukari na viungo kama iliki,vanilla n.k.
0 comments:
Post a Comment
Note: only a member of this blog may post a comment.