Monday 24 November 2014

Faida 7 za kutumia lugha sanifu


Lugha ni nyenzo kubwa sana katika mawasiliano ya kila siku katika jamii. Lugha imewezesha mambo mengi sana akatika jamii zetu kote duniani. Lugha imesaidia sana katika nyanja mbalimbali ikiwemo upashanaji habari,elimu, kusambaza teknolojia na hata kuburudisha. Lugha inatakiwa kutumiwa kwa usahihi kulingana na muktadha mada husika na wazungumzaji pia. Kila jamii ina lugha yake na hakuna lugha iliyo bora kuliko lugha nyingine. Kutokujua matumizi sahihi ya lugha unayoitumia husababisha madhara makubwa katika mawasiliano ya kila siku.Mathalan utumiaji mbovu wa maneno,uandishi usio sahihi na hata matamshi mabovu ni makosa makubwa ambayo hufanywa kila siku na watumiaji wa lugha husika, hivyo kupelekea kutoa ujumbe tata kwa mlengwa/walengwa wako. Katika lugha ya uandishi vituo pia ni muhimu mfano nukta,mkato,alama ya kuuliza nk.
1.Kufikisha ujumbe uliokusudiwa kwa usahihi
Ili uweze kueleweka kwa urahisi ni muhimukutumia maneno yote ya lugha husika kwa usahihi bila kubadili matamshi ama maandishi sahihi ya maneno ili
kuweza kufikisha ujumbe uliokusudiwa kwa mlengwa. Mathalani kutumia ufupisho wa maneno usioeleweka,matamshi mabovu mfano matamshi kulingana  na lugha mama ambayo mara nyingi kwa kiswahili ni s na z,th na dh,r na l ambayo mara nyingi huleta mkanganyiko kwa msikilizaji. Hili tatizo hutokana zaidi na lugha za makabila na mazingira ya kuishi. Haya huwafanya baadhi ya watu kutokujua ni wapi pa kuweka maneno hayo kw usahihi na kuonekana kana kwamba hawaijui lugha husika. Pia matumizi ya mitandaoyamewafanya watu wengi kutumia lugha fupi (text language) ambayo yamewaathiri katika matumizi sahihi ya maneno mfano herufi h watu wengi wamekuwa wakiiondoa ama kuiweka sehemu isiyo sahihi, mfano atawakuta akiwa na maana ya hatawakuta bila kujua kuwa amefikisha ujumbe usio sahihi kwa muhusika. Makosa haya yanaathiri hadi lugha ya Kiingereza.
2.Kujiamini
Matumizi sahihi ya lugha hukufanya ujiamini na hata kuweza kuwasilisha ujumbe kwa jamii.Kutokujua lugha sanifu kumewafanya watu kushindwa kujiamini mbele za watu hasa wajuzi wa lugha husika kwa kuogopa kukosolewa. Pia watu wengine watachukulia kwamba hujui unachokiwasilisha kwa sababu tu hujui lugha sanifu ama kuonekana limbukeni.
3. Hujenga heshima mbele ya jamii
Ni kweli kwamba kuijua lugha fulani kwa usahihi ni heshima mbele za jamii kwamfano mtu anaejua kuongea na kuandika vizuri lugha mbili taifa hili yaani kswahili ama kiingereza hujijengea heshima mbele ya jamii na kutoonekana kutojua lugha husika ama kutoonekana mtovu wa nidhamu kwa kutumia lugha isiyo sahihi mbele ya watu wenye heshima, mfano lugha ya mtaaani kuitumia katika sehemu rasmi.

4.Kuweza kuitumia katika sehemu rasmi
Mazoea ya kutumia lugha za mitaani ama lugha za ufupisho (text language) zimewafanya watu kushindwa kutumia lugha sanifu hasa pale wanapokuwa katiaka sehemu rasmi na kupelekea wengine kukosa fursa muhimu maishani mfano kazi,ama kusikilizwa.mfano wa sehemu rasmi ni kama ofisini,kanisani ama msikitini.
5.Huonyesha kwamba wewe ni mtu makini(unaefanya vitu kwa umakini)
Kutumia kwako kwa ufasaha kunaonyesha kwamba wewe ni mtu unaejali na makini katika kufanya kazi zako,kukosea hutokea lakini si kwa kila sehemu na kila wakati na wakati mwingine bila kujua kama umekosea ama la. Kukosea mara nyingi huonyesha kwamba wewe ni mzembe na uliekosa umakini.
6.Husaidia katika uandishi
Hukusaidia sana katika uandishi wako, mathalani kwenye mitihani,makala,barua na hata vitabu. Kutokujua kwako lugha sanifu kutafanya ujumbe wako usifike kama ulivyokusudiwa ama kuleta mkanganyiko. Kutumia lugha mbovu kutafanya ulichoandika kikose wasomaji.
7.Kuvutia wasilizaji
Ujuvi wa lugha yoyote huleta huleta msisimko na mvuto kwa msilizaji wa lugha husika. Huleta burudani sana ,mfano ni Mrisho Mpoto anapoimba mashairi yake kwa lugha sanifu ya Kiswahili.
Nini cha kufanya?
        i.            Kutafuta usahihi wa maneno yanayokutatiza kwenye kamusi.
      ii.            Kuuliza watumiaji wengine wa lugha husika usipopaelewa.
    iii.            Kutokuchoka kujifunza.
     iv.            Kujijengea mazoea ya kutumia lugha sanifu unapoandika ama unapoongea.
       v.            Kuwa makini na matumizi ya lugha kulingana na mahali na wahusika.
     vi.            Kukubali kukosolewa na kurekebishwa pale unapokosea.

0 comments:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.