Tatizo la uzito mkubwa limekuwa kubwa miongoni mwa jamii
yetu. Tatizo hili linachangiwa kwa kiasi kikubwa na ulaji mbovu usiozingatia
kanuni za afya. Kukubali kwamba una uzito mkubwa ni nusu ya kulitatua tatizo
lako. Ili kujua kama una uzito mkubwa ni lazima uchukue kipimo kinachitwa
BMI (Body mass index). Hichi ni kipimo cha uwiano kati ya uzito wako na urefu wako. BMI hupatikana kwa kwa kugawanya uzito wako kwa urefu wako uliozidishwa kwa wenyewe (squared) katika mita. Yaani uzito gawanya kwa urefu wako. BMI zaidi ya 24.9 huonyesha kwamba uzito wako ni mkubwa na chini ya 18.5.
BMI (Body mass index). Hichi ni kipimo cha uwiano kati ya uzito wako na urefu wako. BMI hupatikana kwa kwa kugawanya uzito wako kwa urefu wako uliozidishwa kwa wenyewe (squared) katika mita. Yaani uzito gawanya kwa urefu wako. BMI zaidi ya 24.9 huonyesha kwamba uzito wako ni mkubwa na chini ya 18.5.
1.
Kula taratibu
Inashauriwa kula mlo wako taratibu. Hutakiwi kula haraka
haraka kwani itafanya ule chakula zaidi ya unachohitaji na kuongeza tatizo la
uzito. Ukila taratibu itachukua kati ya dakika 20-30 kwa ubongo wako kuonyesha
dalili ya kushiba.
2.
Kula tu pale unapohisi njaa
Hii itakusaidia kuepuka kukusanya kiasi kikubwa cha nishati
kama utakula bila kuhisi njaaa. Pia usile ukiwa na msongo wa mawazo, upweke au
unapojihsi kuchukizwa.
3.
Kula vyakula bora
Watu wengi wanaotaka kupunguza uzito wamekuwa wakila vyakula
vsivyo bora, yaani vyenye virutubisho vichache. Hii siyo sahihi hata kidogo.
Kuwe na matunda, mboga, protini na hata wanga.
4.
Kula matunda na mboga
za majani
Unahitajika kula kwa wingi mboga za majani na matunda kwani yana maji mengi na nyuzinuzi lishe (fibres)
ambazo ni muhimu kiafya kwani hsaidia kujaza tumbo na kuepuka ulaji wa mara kwa
mara. Pia husaidia kuondoa mafuta
(lehemu) yasiyohitajika mwilini (bad cholesterol).
5.
Kula vyakula vya
protini kwanza
Vyakula vyenye asili ya protini husaidia kushiba haraka na
pia kufanya tumbo likae muda mrefu bila kula na hivyo kujiepusha na nishati
kubwa kwa kila mlo unaozidi. Pia katika kula angalia kula vyakula katika muda
kamili na paia kutokula nyama zenye mafuta mengi.
6.
Kula bila vizuizi
Unapokula hakikisha kwamba unakula katika hali ya ‘kurelax’
bila vikwazo vyovyote. Unashauriwa kuangalia zaidi katika mlo wako na uache
shughuli zingine hadi utakapomaliza kula. Unatakiwa kuzima TV, kuacha kusoma
magazeti, vitabu naa hata kujifunza. Hii itasaidia sana katika kuridhika mapema
na pia kudhibiti ulaji wako.
7.
Penda unachokula
na furahia mlo wako
Kula vyakula unavyopenda kutakusaidia kushiba mapema na pia.
Kula kwa hisia zote hutoka na mvuto uliopo katiaka chakula hicho kama harufu
nzuri, ladha na hata hali ya ulaini au ugumu wa chakula (texture). Mvuto huu
utakufanya uhisi shibe mapema.
8.
Pata usingizi wa
kutosha
Mtu mzima anashauriwa kulala katika ya saa 7-8 kwa siku. Hii
inashauriwa kwa ajili ya afya bora ya mwili na pia akili.
9.
Kunywa maji ya
kutosha
Hakikisha unakunywa maji ya kutosha kila siku kwa ajili ya
uyeyushaji na usafirishaji wa chakula. Kumbuka maji yana kazi nyingi sana
mwilini. Unashauriwa kunywa angalau glasi nane za maji safi kwa siku. Jiepushe
na vinywaji vye sukari na vyenye caffeine kwani vitafanya uzito wako
kuongezeka.
10.
Fanya mazoezi ya
viungo
Mazoezi ya viungo kila siku ni kitu kisichoepukika kwa afya
bora. Mazoezi mepesi kama kukimbia, kuruka
kamba na hata kichura na mengine mepesi hushauriwa. Hushauriwi kufanya mazoezi
magumu mithili ya wacheza miereka (wrestling).
11.
Usiruke milo/Don’t
skip meals
Hakikisha unakula milo yako yote ya siku bila kuiruka na kwa
muda sahihi. Kuruka milo kutakufanya ujihisi njaa kali na hivyo kulazimika kula
chakula kingi. Watu wengi wamekuwa wakidhani njia ya kuruka milo sahihi ni
sahihi lakini si kweli. Hivyo basi zingatia muda wako wa kula na milo yako ya
kawaida kwa siku.
Asante
kwa kusoma Makala hii.
Karibu
kwa maoni, ushauri na nyongeza.
0 comments:
Post a Comment
Note: only a member of this blog may post a comment.