Katika hali ya kawaida watu wengi wamezoea kusikia na kuambiwa kuwa
Chocolate si kitu kizuri na kuna sababu nyingi za kukufanya uamini kuwa
chocolate si nzuri.
Watu husema inaharibu meno, wengine hudai kuwa
inasababisha kisukari na wengine huenda mbali zaidi wakidhani kuwa inaharibu ngozi
kutokana na wingi wa mafuta iliyo nayo.
Watoto wadogo ambao wamezoeleka kuwa wapenzi wakubwa wa
chocolate ndio huvunjwa moyo na wazazi/walezi wao katika hili.
Ukweli ni kwamba Chocolate si mbaya kwa afya yako na hii
inatokana na matokeo ya utafiti rasmi (research) ambayo yamekuja na faida hizi
nne ambazo zitakufanya ule chocolate mara nyingi zaidi uwezavyo.
1.Chocolate ni nzuri kwa Moyo wako.
Utafiti unaonyesha kuwa chocolate inaweza kusaidia kupunguza
magonjwa ya moyo na hata shinikizo la damu na shambulio la moyo (Heart Attack).
Chocolate nyeusi zimethibitika kuwa na uwezo wa kusaidia
moyo ambao umeanza kuathirika na matatizo ambayo yanaweza kukuletea ugonjwa wa
kiungo hicho muhimu kwenye mwili wa binadamu.
2.Inapunguza kisukari.
Ni vigumu kuamini lakini ukweli halisi ni kwamba , chocolate
inasaidia kuondoa uwezekana wa mtu kupata kisukari.
Watu ambao wamekuwa na kawaida ya kula chocolate walau
kipande kidogo mara moja kwa siku kwa muda wa siku tano wanakuwa na uwezo wa
kuwa na kinga dhidi ya kisukari kuliko wale ambao hawali chocolate kabisa.
3.Kupambana dhidi ya Msongo wa mawazo (stress).
Tafiti za kisayansi zimethibitisha kuwa chocolate inasaidia
kupunguza msongo wa mawazo au stress.
Watu wenye msongo wa mawazo hushauriwa kula walau
gramu 45 za Chocolate kila siku wa muda wa wiki mbili ili kushusha msongo wa
mawazo.
Chocolate hushusha kiwango cha Homoni ya Cortisol mwilini,
homoni hii huongeza au kupunguza msongo wa mawazo.
4.Chocolate husaidia kujikinga dhidi ya Jua.
Chocolate husaidia ngozi ya mawadamu kujikinga dhidi ya
madhara ya miale ya jua.
Flavonoids ambazo zinatumika kutengeneza chocolate zina
chembechembe ya vimelea (microorganisms) vinavyoweza kusaidia ngozi na kuikinga
dhidi ya miale ya jua.
Asante kwa kusoma makala hii fupi.
0 comments:
Post a Comment
Note: only a member of this blog may post a comment.