Katika makala iliyopita tuliona
jinsi marafiki walivyo muhimu katika maisha yetu. Hivyo basi leo nimeona ni
bora nijaribu kueleza namna ya kuwa rafiki bora. Ili kuwa rafiki bora huna
budi;
1. Jifunze kusamehe
Kama ilivyo kwa penseli kuwa na ufuto ndivyo na marafiki walivyo. Katika dunia hii hakuna mtu yeyote aliye
mkamilifu. Kama ni hivyo basi kila mtu hutenda makosa na kama kama anakosea
basi yapasa kusamehewa ili maisha yasonge mbele. Hupaswi kuwa na kinyongo.
Samehe na sahau kabisa kwani msamaha bila kusahau ni sawa na kulima shamba bila
kupalilia. Kama ilivyo safari ambayo hupitia milima na mabonde mingi ndivyo
ulivo urafiki. Kadiri mtakavyokaa pamoja na kusameheana mengi ndivyo na urafiki
wenu utakavyostawi.
2. Kuwa msikilizaji
mzuri
Kila mtu anahitaji kusiilizwa.
Kama ambavyo wewe ungependa kusikilizwa ndivyo na rafiki yako anavyotaka
asikilizwe na wewe. Ili kujenga urafiki imara basi jiandae kusikilza marafiki
zako na inapobidi kuwasaidia.
3. Wekeza katika
urafiki wenu
Kama shamba linavyohitaji matunzo
ndivyo na urafiki unavyohitaji malezi. Unapaswa kutafuta kitu ambacho mnapenda
kukifanya kwa pamoja hata kama utakuwa umetingwa sana na kazi ama una msongo
angalau mara moja kwa wiki. Mfano
mnaweza kukaa sehemu tulivu na kubadilishana mawazo, kutembelea mbuga za
wanyama, kucheza/kuangalia pamoja mchezo mnaoupenda na hata kutembeleana na
mengine mengi.
4. Kuwa kama rafiki
unayemtaka
Mtendee rafiki yako kadiri wewe
unavyotaka kutendewa. Maana yake mtendee rafiki yako mambo mema, mambo ambayo
hata wewe ungependa kutendewa. Kumbuka hakuna mtu anayependa kutendewa mambo
mabaya.
5. Usimbane sana rafiki
yako.
Usimbane sana rafiki yako kwamba
muda wote muwe pamoja bali mpe nafasi aamue mwenyewe. Atahitaji kuwa na watu
wengine tofauti na wewe. Pia usiwe tegemezi sana kwake kwani utahatarisha
urafiki wenu. Pia usiweke masharti magumu katika urafiki wenu bali acha urafiki
wenu ukue katika ya hali yake ya asili kwani ukiulazimisha utakufa siku moja.
Asante na karibu kwa maoni, ushauri na nyongeza
0 comments:
Post a Comment
Note: only a member of this blog may post a comment.