Maisha ni jinsi unavyoyachukulia
mwenyewe. Maisha bora unayaandaa mwenyewe. Kuwa na maisha bora na ya furaha
kuna vitu ambavyo unatakiwa kuwa navyo. Vitu hivyo huwezi kuletewa na mtu
yeyote isipokuwa wewe mwenyewe. Huhitaji pesa, umaarufu ama madaraka ili uwe na
maisha bora na furaha. Simaanishi kwamba pesa, madaraka au umaarufu
havihitajiki maishani la hasha, namaanisha kuwa kuwa navyo bila kufanya haya ni
ngumu kuwa na maisha bora.
Kubadili vitu unavyoweza kubadili
Kubali usikubali kuna vitu
ambavyo unaweza kuvifanya ama kuvibadili maishani, hivi vibadili haraka
iwezekanavyo. Usisubiri aje mtu mwingine avibadili kwani mara nyingi vyote vipo
ndani uwezo wako. Kubadili tabia zako hakuhitaji usaidizi wa profesa wako wa
chuo, bosi wako wala mwenyekiti wako wa mtaa. Je huwezi kubadili tabia yako ya
uvivu? Huwezi kubadili tabia yako ya ufujaji wa pesa? Huwezi kuamua kuwa na
mafanikio? Huwezi kuwa mwekezaji? Bila shaka tabia hizo na nyinginezo nyingi ziko
ndani ya uwezo wako na ukiamua kubadili hakika