Monday, 4 July 2016

Choma meli yako sasa

Ndugu msomaji napenda kutumia wasaa huu kuweza kukusalimia kabla sijaanza kukushirikisha niliyonayo leo. Nianze kwa kukusimulia hadithi moja:

Hapo zamani kuna kiongozi wa nchi fulani alienda vitani na jeshi lake katika nchi ya kigeni kwa kutumia usafiri wa meli. Alipofika pwani ya nchi ya adui aliamuru jeshi lake kuchoma meli waliyokwenda nayo. Aliwaambia wapiganaji wake kwamba kwa sasa wana machaguo mawili tu ambayo ni kushinda ile vita na ni lazima washinde ama kufa wote kwani hawawezi kutoka salama huko kwa kutoroka kwani wameshachoma moto meli yao. Wasiposhinda maana yake watauawa ama watakuwa mateka ama washinde vita na warudi nchini kwao salama. Hapo sasa kukawa hakuna jinsi zaidi ya jeshi lake kuwa na dhamira moja tu ya kushinda