Monday 4 July 2016

Choma meli yako sasa

Ndugu msomaji napenda kutumia wasaa huu kuweza kukusalimia kabla sijaanza kukushirikisha niliyonayo leo. Nianze kwa kukusimulia hadithi moja:

Hapo zamani kuna kiongozi wa nchi fulani alienda vitani na jeshi lake katika nchi ya kigeni kwa kutumia usafiri wa meli. Alipofika pwani ya nchi ya adui aliamuru jeshi lake kuchoma meli waliyokwenda nayo. Aliwaambia wapiganaji wake kwamba kwa sasa wana machaguo mawili tu ambayo ni kushinda ile vita na ni lazima washinde ama kufa wote kwani hawawezi kutoka salama huko kwa kutoroka kwani wameshachoma moto meli yao. Wasiposhinda maana yake watauawa ama watakuwa mateka ama washinde vita na warudi nchini kwao salama. Hapo sasa kukawa hakuna jinsi zaidi ya jeshi lake kuwa na dhamira moja tu ya kushinda
kwani kwani kwa namna yoyote hawako salama maana wakipigana wanaweza kushinda lakini pia wanaweza kufa na wasipopigana pia wanaweza kufa kwa hiyo walijitoa kwa moyo mmoja na kuamua kupambana na adui. Walishikamana na kuamua kupambana na kwa moyo mmoja na hatimaye wakashinda ile vita. Bila wao kudhamiria kushinda ile vita kamwe wasingeweza kushinda, bila kuchoma meli yao naamini wasingeweza kuishinda vita ile. Kuchoma ile meli ndiyo maamuzi magumu waliyoyafanya na kuamua kuishinda. Kuna kiongozi wa Tanzania aliwahi kusema ``Ni bora kulaumiwa kwa kuchukua maamuzi magumu kuliko kulaumiwa kwa kutochukua maamuzi magumu.´´

Hadithi hii inatufundisha nini mimi na wewe?
Kuendelea kusoma bonyeza maandishi haya Choma meli yako sasa

Ndugu msomaji nimeamua kuhamishia makala zote katika mtandao wangu mpya kwani nina mpango wa kuacha kuandika huku. Bonyeza maandishi ya bluu kuweza kupata mtandao huu mpya

0 comments:

Post a Comment

Note: only a member of this blog may post a comment.