Ili uweze kufanya shughuli zako za kila siku ikiwa ni pamoja
na shughuli za uzalishaji mali ni lazima uwe na afya njema. Afya ni hali ya
kuwa vizuri kimwili, kiakili, kisaikolojia na kiroho pia. Watu wengi huchukulia
kuwa watu wanene ndio wenye afya njema na wakati mwingine hudhani kuwa watu
wembamba ndio wenye afya. Lakini kiukweli hilo si kweli. Mtu mwenye afya ni yule mwenye sifa nilizotaja
hapo juu.

Kama huna mojawapo kati ya hivi
basi hatuwezi kusema kuwa una afya njema. Ukiwa na afya njema utaweza kuishi
maisha yenye furaha na amani na pia utaweza kujizalishia kipato chako kwa kila
siku iendayo kwa Mungu. Ili uwe na afya njema inakupasa
ufanye yafuatayo kila siku kama siyo kila mara. SOMAHizi ndizo kanuni za kuwa na afya njema
ufanye yafuatayo kila siku kama siyo kila mara. SOMAHizi ndizo kanuni za kuwa na afya njema
1. Kula vizuri/kula mlo bora
Ili uwe na afya au siha njema
kama binadamu inakubidi ule vizuri kila siku. Mlo bora si lazima uwe na nyama
kila siku kama wengi wanavyodhani. Sio lazima ule mlo mkubwa sana bali ule
chakula cha kukutosha kila siku. Lazima ule mlo wa kukutosha na si kula chakula
kisichojitosheleza. Kula sana matunda na mboga za majani kila siku ili uweze
kuboresha afya yako. Epuka kuwa na mwili mkubwa kupitiliza kwa hiyo pia kula
kulingana na uzito wa mwili wako. Kumbuka kama hutaweza kula chakula bora kama
dawa kwa sasa basi unajiandaa kula madawa baadae kama chakula. Madhara ya kula
vibaya unaweza usiyaone sasa hivi bali kwa muda mrefu ujao.

2. Fanya mazoezi ya viungo kila mara
Nakushauri kila siku ufanye
mazoezi ya viungo. Kama ratiba imekubana unaweza kutenga siku kadhaa katika
wiki ambazo utatumia kwa mazoezi, pia unaweza kutenga muda mfupi sana wa hata
dakika kumi kila siku. Naamini katika saa 24 za siku huwezi kukosa angalau
dakika kumi za kufanya mazoezi. Faida ya kufanya mazoezi ni kama kuongeza
msukumo wa damu mwilini, kusaidia katika mmeng’enyo w achakula, akili kufanya
kazi vizuri, kupata usingizi mzuri na kadhali. Unaweza kufanya mazoezi mepesi
kila siku kama kukimbia, kuruka kamba na push-ups. Mwanzo utaonekana mgumu
lakini kadiri siku zitakavyoenda utazoea na utakuwa huwezi kukaa bila kufanya
mazoezi. Kumbuka mazoezi husaidia wewe kuwa na nguvu na afya bora katika umri
wowote.


3. Pata usingizi wa kutosha
Katika siku yenye saa 24 tenga
muda wa kutosha wa kuweza kupata usingizi. Jitahidi ulale kwa angalau saa 7
hadi 8 kwa siku kama inavyoshauriwa na wataalamu. Hii itakujengea afya ya akili
na afya ya mwili pia. Utafiti uliofanywa unaonyesha kuwa watu wanaopata
usingizi wa kutosha kila siku hufanya kazi zao vizuri kulinganisha na wale
wasiopata usingizi wa kutosha. Kumbuka mwili wako sio roboti hivyo kulala ni
sehemu ya maisha yako. Hutaweza kumaliza kila kitu kwa kutokulala. Kama wewe ni
mwanafunzi na umebanwa na ratiba za shule tenga muda wa kufanya mambo yako ya msingi
na kuachana na visivyo na msingi kwako. Kama unaingia zamu ya usiku kazini
kwako, basi tenga muda wa mchana kupumzika.

4. Kunywa maji ya
kutosha kila siku
Jenga mazoea ya kunywa maji kila siku. Kunywa maji safi na
ya kutosha kila siku. Usisubiri mpaka uhisi kiu. Nakushauru unywe maji safi
kwani maji ambayo siyo safi na salama huambukiza magonjwa kama kipindupindu,
kuhara, taifod n.k. maji yana faida nyingi mwili kama kupoza mwili kwenye joto,
usafirishaji mwilini, kusafisha mwili kama figo n.k. Ukosefu wa maji mwili una
hasara nyingi kuliko faida. Hakuna kinywaji kinachoweza kuchukua nafasi ya
maji, hivyo basi kaa ukijua kwamba maji yana umuhimu wa kipekee mwilini na ndio
maana zaidi ya robo tatu ya mwili wako ni maji. Hata kama unapenda unapenda
soda au chai usiache kunywa maji kila siku.


5. Punguza msongo wa
mawazo
Msongo wa mawazo ni hali ya akili kulemewa na mawazo mengi
bila kuwa na namna ya kufanya utatuzi. Kama hali ikikutokea haina maana kwamba
ndiyo unatatua tatizo bali unaongeza tatizo kwani hutaipa akili kufikiria namna
ya kutafuta ufumbuzi. Kaa chini fikiria uwezekano wa kutatua tatizo lako, omba
msaada kwa watu wako, mwambie ndugu au rafiki unaemuamini na pia nenda sehemu
nzuri kuweza kupunguza mawazo. Kadiri unavyokuwa na mawazo ndivyo unavyozidi
kuharibu afya yako. Kama huna afya ya saikolojia basi huna afya kwani mwili
wako unaitegemea akili yako kuweza kufanya kazi. Acha kuangalia matatizo yako
bali ona kama changamoto na pia tafuta namna ya kuweza kufanya utatuzi. SOMA Causes effects and management of stress
6. Usitumie vilevi au
madawa ya kulevya
Nakushauri kama unatumia sana
vile punguza au acha kabisa. Kama unakunywa kidogo kama sehemu ya burudani sio
mbaya ila kama unakunywa kama sehemu ya kukimbia matatizo yako basi nakushauri
uache mara moja kwani tatizo halikimbiwi bali hutatuliwa. Kuna watu wmekuwa
wakitumia vilevi na madawa ya kulevya kama sehemu ya maisha yako na sehemu ya
burudani. Kama unalewa mpaka unashindwa kujitambua unapata faida gani hapo? Unapoteza
pesa,unaharibu afya, unaharibu mahusiano na pia unajipotezea heshima mbele za
watu. Kwa upande wa madawa ya kulevya achana nayo kabisa kwani hakuna faida
yoyote unayoipata zaidi ya starehe ya dakika chache ambayo itakuacha ukiwa teja
usiyekuwa na mwelekeo.

Madawa kama bangi, kokein, heroin n.k. Hata sigara kaa nayo mbali. Unaharibu afya ya akili yako na hata afya ya mwili wako, unashindwa kuzalisha mali na pia unajiandalia mazingira ya kuugua saratani hasa unapotumia sigara.
Madawa kama bangi, kokein, heroin n.k. Hata sigara kaa nayo mbali. Unaharibu afya ya akili yako na hata afya ya mwili wako, unashindwa kuzalisha mali na pia unajiandalia mazingira ya kuugua saratani hasa unapotumia sigara.
7. Pata muda wa
kupumzika
Kama nilivyosema hapo juu wewe ni binadamu, kiumbe ambaye unachoka.
Mashine zinachoka na kupumzika sembuse wewe mwanadamu? Tenga muda wa kupumzika
na kutafakari maisha yako. Upe mwili nafasi ya kuweza kujijenga upya na kupata
nguvu mpya. Ila sikushauri upumzike kupitiza kwani huo utakuwa ni uvivu. Kupumzika
baada ya kazi ni vizuri lakini kupumzika kabla au ukiwa hujafanya kazi ni
uvivu. Muda ambao wewe utaupanga kupumzika ni juu yako mwenyewe kuamua. Kumbuka
katika kipindi cha kuupumzisha mwili wako ndipo na mawazo mapya na ya kujenga
huja.
8. Kuwa na furaha na
acha uoga
Hakuna siku ambayo utapanga kuwa na furaha zaidi ya leo. Jana
ni siku ambayo ilishapita na haitarudi tena katika maisha yako yote hivyo kwa
vyovyote isikuaharibie siku njema ya leo. Kesho nayo ni siku usiyokuwa na
uhakika nayo kwa hiyo isikuharibie leo yako. Leo ndio siku ambayo unatakiwa uwe
na furaha na ufurahi kwa kila siku iitwayo leo. Matatizo yasiwe sehemu ya
kukuibia furaha yako. Pia usijiwekee vigezo kwamba nitakuwa na furaha pale
nitakapofanikisha kitu fulani. Pia acha
woga kwani utaharibu maisha na mafanikio yako. Kabiliana na kila tatizo kwa tumaini
kubwa kwani kila tatizo huja na namna yake ya kutatuliwa. Mwisho jua kuwa kama
maisha yako hayana furaha na amani yatakuwa maisha yasiyo na thamani.
Natumaini umejifunza misingi ya afya bora. Najua kuna vitu
vingi kuhusu afya ambavyo sijaandika, natumaini utaendelea kujifunza zaidi ili
uwe na afya njema. Kumbuka afya ndiyo msingi na kipaumbele cha kwanza katika
mafanikio yako

Kwa maoni, ushauri au mapendekezo usisite kuwasiliana nami kwa
e-mail: nmyohanes@gmail.com au kwa
simu namba 0712-843030.
2 comments:
asante kwa ushauri ubarikiwe sana!
ahsante mr
Post a Comment
Note: only a member of this blog may post a comment.